Home Sports MWANZO MBAYA KIMATAIFA IWE NI SOMO KWA VITENDO

MWANZO MBAYA KIMATAIFA IWE NI SOMO KWA VITENDO

WAWAKILISHI wa kimataifa kwenye mechi za kimataifa nyumbani na ugenini hakuna ambaye ameanza kwa mwendo mzuri.Ipo wazi kuwa ni mwendo mbovu wameanza nao kwa kushindwa kupata matokeo.

Kutokana na kuanza hivyo kwa kushindwa kushinda huku wachezaji wakionekana kutotumia nafasi wanazotengeneza ni muhimu kutumia ubovu huo kuwa darasa huru kwenye mechi zinazofuata.

Yanga na Simba katika mechi za kimataifa za hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika kete za Novemba hazijawa na furaha kwao na mashabiki. Simba nyumbani aliambulia pointi moja licha ya kuanza kupata bao la kuongoza.

Yanga wao ugenini walipoteza pointi tatu mazima. Haikuwa wiki nzuri kwa kila upande na matokeo hayakuwa rafiki hasa ukizingatia hesabu zinaanza kupigwa mwanzo.

Ipo wazi kwamba wachezaji wanapenda kuona timu inapata matokeo mazuri hata benchi la ufundi pia mpaka mashabiki. Ikawe hivyo kwa vitendo isiishie kwenye kufikiria tu.

Kwa yote yaliyotokea ni muda wa kufanyia kazi mapungufu kwa wachezaji na benchi la ufundi. Wachezaji mnatakiwa kujituma na kufanya kweli katika kutafuta matokeo.

Bendera ya Tanzania inapeperushwa na wachezaji wote kitaifa na kimataifa. Mechi zijazo kukawe na ari mpya na kasi mpya kwenye kutafuta matokeo uwanjani.

Kila la kheri wawakilishi wetu Simba na Yanga kwenye mechi za kimataifa, fanyeni kweli iwe ni nyumbani ama ugenini inawezekana.

Previous articleSIMBA WASIKITIKIA MATOKEO YAO KIMATAIFA
Next articleBODI YA FILAMU YAKAMILISHA MCHUJO TUZO 2023