KOCHA ALIYETIMULIWA SIMBA ATAJA TATIZO LILIPO

Mchambuzi Nguli wa maswala ya soka nchini Saleh Ally Jembe amesema kuwa alipata bahati ya kuonana na aliyekuwa kocha mkuu wa Simba, Roberto Oliveira na kutaja tatizo lilipo.

Ikumbukwe kwamba Oliveira alikuwa ndani ya kikosi cha Simba alipochukua mikoba ya Zoran Maki ambaye alibwaga manyanga muda mfupi baada ya kuwa na timu hiyo.

Mchezo wa mwisho kwa Oliveira kukaa benchi ilikuwa ni Novemba 5 2023 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 1-5 Yanga.

Ulikuwa ni mchezo wa kwanza kwa Simba kupoteza msimu wa 2023/24.

Jembe ameweka wazi kuwa amekutana na aliyekuwa kocha wa klabu ya Simba Robertinho akiwa kwenye gari maeneo ya Msasani Dar alipata muda wa kupiga nae stori, Robertinho amekili tatizo kubwa kwenye klabu ya simba ni wachezaji na uongozi wa klabu hiyo wanapaswa kurekebisha makosa mengi yaliyopo klabuni hapo.

Pia Robertinho ameonesha kufurahi na aliweza kugonga mikono na mashabiki wa klabu ya Yanga.

Video kamili ipo YouTube channel yetu Global Tv Online