Home Sports GAMOND AJA NA JAMBO HILI KUHUSU WAFUNGAJI

GAMOND AJA NA JAMBO HILI KUHUSU WAFUNGAJI

MIGUEL Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga, amesema kuwa hawapi majukumu washambuliaji pekee kufunga ndani ya kikosi hicho bali kawapa uhuru wachezaji wote kufunga.

Ikumbukwe kwamba, Yanga ini namba moja kwa kufunga mabao mengi ikiwa imetupia mabao 26 baada ya kucheza mechi 9.

Gamondi amesema kuwa wachezaji wote wana kazi ya kutafuta matokeo uwanjani, hivyo ni lazima watumie nafasi ambazo wanazipata bila kujali anacheza nafasi gani.

“Unaona kwenye mabao mengi ambayo tunafunga washambuliaji wetu hawajafunga mabao mengi. Ipo hivyo kulingana na namna ambavyo wachezaji wanashirikiana kwenye kutimiza majukumu.

“Viungo wanafunga mabao kwenye mechi wanazocheza, mabeki nao wanafunga hivyo kila mchezaji kwenyetimu ana uhuru wa kufunga ili kuipa timu matokeo kikubwa ni pointi tatu muhimu na kucheza vizuri,” amesema Gamondi.

Previous articleMKWANJA MREFU ATAKUJA TEN HAG
Next articleKOCHA ALIYETIMULIWA SIMBA ATAJA TATIZO LILIPO