Home Uncategorized HIVI NDIVYO MGAWANYO ULIVYO, POTI ZA SIMBA NA YANGA KIMATAIFA

HIVI NDIVYO MGAWANYO ULIVYO, POTI ZA SIMBA NA YANGA KIMATAIFA

MIGUEL Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga amekiongoza kikosi hicho kutinga hatua ya makundi baada ya miaka 25.

Atakuwa shuhuda wa kujua kundi atakalokuwa leo Oktoba 6 jijini Johannesburg, Afrika Kusini ikiwa ni tukio la kupangwa kwa droo ya hatua ya makundi kimataifa kwa Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika.

Kwa Simba ni Kocha Mkuu, Roberto Oliveira atakuwa shuhuda wa kuwatambua wapinzani wake kwenye anga la kimataifa.Timu mbili kutoka ardhi ya Tanzania zipo hatua hiyo ikiwa ni Yanga na Simba.

Poti zipo nne kuendana na wingi wa poiñti ambazo timu hizo 16 zumekusanya katikà michuano ya kimataifa.

Poti 1

Al Ahly, Mamelodi, Esperance, Wydad Casablanca.

Poti 2
Simba, CR Belouzdad, Petro Atletico, Pyramid

Poti 3
Yanga, TP Mazembe, ASEC Mimosas, Al Hilal

Poti 4

Jwaneng Gallaxy, Medeama, Etoile Du Sahel, FC Nouadhibou.

Previous articleKISA PIRA PAPATUPAPATU, SIMBA YABADILI GIA
Next articleFAHAMU BINGWA WA KOMBE LA DUNIA HULIPWA PESA HIZI