UONGOZI wa Yanga umesema ligi bado ndefu hivyo bado nafasi ipo kufanya vizuri mechi zinazofuata.
Oktoba 4,2023 ubao wa Uwanja wa Highland Estate ulisoma Ihefu 2-1 Yanga.
Ikumbukwe kwamba msimu wa 2022/23 kwenye mchezo wa ligi ambao Yanga ilicheza ugenini dhidi ya Ihefu ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1.
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema: “Bado ligi ni ndefu, tumecheza mechi nne. Kweli tumepoteza lakini bado ligi inaendelea na kuna mechi 30 za kuchezwa mpaka sasa ni nne tumecheza.
“Ni sehemu ya matokeo ambayo yanapatikana kwenye ligi hivyo mashabiki wasikate tamaa wazidi kuwa pamoja nasi kwa kuwa kuna mechi za kucheza na tunaamini tutapata matokeo chanya,”.
Kikosi cha Yanga kimewasili Dar kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao ujao wa ligi ambao utakuwa dhidi ya Geita Gold.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.