Azam FC kamili kimataifa

Kocha wa Azam, Florent Ibenge amesema kuwa hataki kuona makosa waliyoyafanya katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya AS Meniema ya DR Congo yakijirudia kwa Wydad Casablanca ya Morocco.

Katika mchezo wa kwanza ugenini wawakilishi wa Tanzania kimataifa walipoteza pointi tatu muhimu kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Baada ya dakika 90 ubao ulisoma AS Maniema 2-0 Azam FC hivyo mchezo wa leo unakuwa wa pili kwenye hatua ya makundi kwa Azam FC na mchezo wa kwanza wakiwa nyumbani.

Ibenge amesema kuwa kilichomgharimu mchezo dhidi ya AS Maniema ni kikosi chake kutokucheza kwa utulivu na umiliki mdogo wa mpira huku wakipoteza pasi nyingi katika dakika 45 za mwanzo.

“Hatutaki kuona tukirudia makosa tuliyoyafanya katika mchezo uliopita dhidi ya Maniema. Tunajua kwamba mchezo uliopita tulipoteza.

“Makosa ambayo tulifanya kwenye mchezo huo tuliangalia kwa mara nyingine mechi na kufanyia mazoezi makosa ili kuwa imara tunaamini mchezo wetu utakuwa na ushindani lakini tupo tayari,”.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.