Home International HAWA HAPA WALIOPIGA HAT TRICK KWA HARAKA ZAIDI

HAWA HAPA WALIOPIGA HAT TRICK KWA HARAKA ZAIDI

Soccer Football - Champions League - Quarter Final - First Leg - Manchester City v Bayern Munich - Etihad Stadium, Manchester, Britain - April 11, 2023 Manchester City's Erling Braut Haaland celebrates scoring their third goal REUTERS/Molly Darlington

KUFUNGA mabao matatu ‘hat trick’ ndani ya mchezo mmoja sio kitu rahisi. Washambuliaji wengi wamekuwa na ndoto ya kufanikisha hilo na wengine hadi wanastaafu wanakuwa hawajafanikiwa kutimiza.

Premier League ni kati ya ligi zinazofuatiliwa kwa kiasi kikubwa ulimwenguni. Hii imepelekea klabu za huko kusajili wachezaji wazuri hususan washambuliaji wenye uwezo mkubwa kucheka na nyavu kila wikiendi.

Hapa kuna listi ya wachezaji watano ambao wamefanikiwa kupiga hat trick tano baada ya mechi chache zaidi kama kawaida Erling Haaland anaongoza akiwa na msimu mmoja tu.

5 Harry Kane – 115 games

Harry Kane amefunga mabao 213 Premier katika mechi 320 alizocheza. Staa huyo ameondoka kwa sasa Premier na kwenda Bundesliga ambako amejiunga na klabu ya Bayern Munich akitokea Tottenham.

Kane ndiye mchezaji anayeshika nafasi ya pili kwenye listi ya wafungaji bora wa muda wote Premeir nyuma ya Alan Shearer tangu ligi hiyo ilipobadili mfumo wao mwaka 1992.

Kabla ya kujiunga na miamba hiyo ya Ujerumani majira haya ya joto, straika huyo wa kati ana rekodi ya kufunga hat trick tano baada ya mechi 115 tu.

  1. Alan Shearer

Mfungaji bora wa wakati wote Premier, nyota huyu aliyecheza Newcastle United na Blackburn Rovers anaongoza kwa mabao kwenye ligi hiyo kwa miaka yote akitupia 260 katika mechi 441. Pia amepiga asisti 64, alistaafu baada ya misimu 14 kwenye soka la kulipwa huko England.

Ndani ya muda wote huo, amefanikiwa kufunga hat trick tano baada ya mechi 110.

3 Luis Suárez

Staa huyu mwenye umri wa miaka 36 kwa sasa yuko nje ya Ulaya akikipiga kunako klabu ya huko Brazil, Grêmio Foot-Ball Porto Alegrense, baada ya kucheza kwa miaka mitatu na nusu England.

Alisajiliwa Januari 31, pale Liverpool wakati klabu hiyo ikitambulisha mastraika wawili siku ya mwisho ya usajili, mwingine alikuwa Andy Carroll aliyetokea Newcastle United huku Suárez akitokea Ajax.

Suarez alisajiliwa kwa ajili ya kuwa mbadala wa Fernando Torres. Suarez alicheza mechi 133 kabla ya kutimkia Barcelona. Akiwa Liver, Suárez alifunga hat trick tano kwenye Premier League baada ya mechi 86.

2 Ruud van Nistelrooy

Ruud van Nistelrooy hakufunga zaidi ya hat trick tano pale Premier League lakini ni mmoja kati ya wachezaji nyota kwa miaka hiyo. Majira ya joto mwaka 2001, Manchester United walitangaza usajili wa Mholanzi huyu akitokea PSV Eindhoven kwa ada ya rekodi Uingereza ya pauni mil 19.

Ndani ya miaka mitano aliyokuwa Old Trafford, alifanikiwa kufunga mabao 150 na ilimchukua michezo 73 tu kufanikiwa kupiga hat trick tano na kuwa ndiye mchezaji aliyefunga idadi hiyo ya hat trick kwa haraka zaidi kabla ya mwamba pale jirani yao kuvunja rekodi yake.

 1 Erling Haaland

Ukiwa ni msimu wake wa kwanza tu England, mwamba kutoka Manchester City, Erling Haaland alibadilisha kila kitu na kuvunja rekodi kibao za mabao Premier League.

Haaland ambaye amejiunga na City majira ya joto mwaka 2022 akitokea Borussia Dortmund kwa sasa anashinda nafasi ya kwanza kati ya nyota waliopiga hat trick tano ndani ya muda mfupi tu.

Haaland aliyesajiliwa kwa pauni 51.2 milioni ameshafunga hat trick tano tu ndani ya mechi 39, moja ya hat trick zake akiifunga Manchester United na kuweka pia rekodi ya kufunga hat trick tatu za haraka zaidi akifikia rekodi ya staa wa zamani wa United, Michael Owen.

Owen ilimchukua mechi 48 kufunga hat trick tatu.

 

Previous articleHILI HAPA BALAA LA YANGA KITAIFA NA KIMATAIFA
Next articleUSITUPE NGUVU ZAKO BURE KUONYESHA TFF YA KARIA HAIJALETA AFCON TANZANIA