KUELEKEA mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga dhidi ya Al Merrikh, Waarabu hao wa Sudan watakutana na balaa jipya linalosukwa na Miguel Gamondi ambaye ni Kocha Mkuu wa Yanga.
Gamondi anaandaa zana za kazi kuelekea mchezo huo muhimu kwa Yanga kupata ushindi kukata tiketi ya kutinga hatua ya makundi Afrika.
Mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Septemba 30, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar, utatoa mshindi wa jumla atakayekata tiketi ya kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.
Gamondi amesema kila mchezo una mbinu tofauti kulingana na aina ya wapinzani jambo linalofanya wabadili mara kwa mara.