Home Sports MWAMBA SKUDU AMPA NGUVU GAMONDI

MWAMBA SKUDU AMPA NGUVU GAMONDI

SKUDU Makudubela ingizo jipya ndani ya kikosi cha Yanga limeogeza nguvu katika kikosi hicho kinachoongoza ligi baada ya kukusanya pointi sita na mabao 10.

Makudubela hakuwa katika mechi hizo mbili za ligi za ushindani ambazo ni Yanga 5-0 KMC na Yanga 5-0 JKT Tanzania kutokana na kutokuwa fiti baada ya kupata maumivu kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC.

 Kocha Mkuu wa Yanga, Migueli Gamondi amesema kuwa kurejea kwa Skudu uwanja wa mazoezi unaongeza nguvu ya kuwa na chaguo la nani aanze kikosi cha kwanza.

“Skudu hakuwa nasi kwa muda kutokana na kutokuwa fiti lakini kwa sasa maendeleo yake ni mazuri na ameanza mazoezi na wachezaji wenzake hilo linaongeza nguvu wenye kikosi chetu.

“Ukiwa na wachezaji wengi ambao wapo tayari kwa mchezo wanaongeza ukubwa wa kuamua nani ataanza kwenye mchezo husika kikubwa ambacho kinafurahisha ni kwamba wachezaji wote wapo tayari,” amesema Gamondi.

Previous articleMAPUMZIKO YA DHAHABU YASIDUMAZE USHINDANI
Next articleUKUBWA WA SIMBA UMESHAFAHAMIKA