Home Sports MAPUMZIKO YA DHAHABU YASIDUMAZE USHINDANI

MAPUMZIKO YA DHAHABU YASIDUMAZE USHINDANI

WAKATI wa mapumziko kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara ni muhimu kuwa na manufaa kwa kila mmoja kuanzia benchi la ufundi mpaka wachezaji.

Tumeona kabla ya ligi kusimama kuna baadhi ya timu ambazo zilikuwa kwenye mwendelezo mzuri wa kupata matokeo chanya.

Haina maana mapumziko haya yawatoe kwenye ile kasi haitapendeza bali ni muhimu kuendelea pale ambapo mliishia ligi itakaporejea.

Kila timu inahitaji matokeo mazuri kwenye mechi zake zote na haya ili yatokee ni muhimu kila mmoja kutimiza majukumu yake kwa wakati.

Wapo wachezaji ambao wamesharejea kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi zinazofuata na wengine wapo kwenye majukumu ya timu ya taifa.

Ambao bado likizo haijagota mwisho wanapaswa kufuata program ambazo watakuwa walipewa na benchi la ufundi ili wazidi kuimaraisha viwango vyao.

Ligi ikirudi kazi inapaswa kuendelea kwa kuwa ukurasa wa ushindani upo mwanzo. Ili kuwa na mwendelezo mzuri ni muhimu kufanya maandalizi mazuri.

Benchi la ufundi kwa mechi hizi za mwanzo kuna mapungufu ambayo yameonekana hapo ni muhimu kufanyia kazi.

Ikiwa kila mmoja atatimiza majukumu yake kwa wakati likizo hii itakuwa na manufaa makubwa kwa kila mmoja ambaye atatimiza kile kinachostahili.

Wale ambao watapuuzia ukweli utakuwa wazi kwani mpira haufichiki ni mchezo wa wazi kila kitu kitaonekana ndani ya dakika 90.

Previous articleBOSI SIMBA: AL AHLY NDIO TULIKUWA TUNAWATAKA, YANGA YAVUJISHA SIRI
Next articleMWAMBA SKUDU AMPA NGUVU GAMONDI