Home International ISHU YA SALAH KUUZWA UARABUNI IPO HIVI

ISHU YA SALAH KUUZWA UARABUNI IPO HIVI

JURGEN Klopp amesema kuwa Liverpool bado hawajapokea ofa kutoka Saudi Arabia kwa ajili ya Mohamed Salah, huku akisisitiza kuwa staa huyo ambaye amejitolea kwa 100% klabuni hapo hauzwi.

Salah, 31, anawavutia mabingwa wa Saudi Pro League, Al Ittihad, ambao wanaripotiwa kuandaa dau la pauni milioni 100 ili kumng’oa Anfield majira haya ya joto.

Hata hivyo Liverpool wamesisitiza kwamba mshambuliaji huyo wa Misri hauzwi, akiwa ametoka kusaini mkataba wa miaka mitatu na Majogoo hao msimu uliopita ambao utamweka Anfield hadi mwaka 2025.

Klopp amekaririwa akisema kwamba Mo Salah hataondoka na wala hauzwi.

“Al Ittihad? Hatuna ofa – Mo Salah ni mchezaji wa Liverpool, kwa mambo yote tunayofanya ni muhimu. Ikiwa kungekuwa na kitu, jibu litakuwa HAPANA.

“Mo, amejitolea kwa 100% kwa Liverpool. Hakuna cha kuongea, yeye ni mchezaji wetu kwa hivyo hakuna cha kusema.”

Kocha wa Al Ittihad ambaye ni gwiji wa Liverpool, Steven Gerrard aliulizwa kama angependa kumsajili Salah, alicheka kisha akasema: “Hapana! Jibu ni hapana kwa sababu Mohamed Salah ni mchezaji ninayempenda, naipenda Klabu ya Liverpool, hivyo Mohamed anaweza kubaki pale alipo.”

Baadhi ya ripoti zinaonyesha kuwa Al-Ittihad itakuwa tayari kulipa ada ya uhamisho ya karibu pauni 100m na kumlipa mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri mshahara wa karibu  pauni 200m kwa mwaka ikimaanisha kuwa angelipwa hata zaidi ya pauni 3.4m za Ronaldo kwa wiki bila kodi.

Previous articleAZAM FC YATAJA SABABU YA KUKWAMA KIMATAIFA
Next articleKIKOSI CHA YANGA DHIDI YA ASAS LIGI YA MABINGWA AFRIKA