Home Sports YANGA YAJA NA HESABU NYINGINE

YANGA YAJA NA HESABU NYINGINE

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi ameweka wazi kuwa mchezo wa mpira unahitaji mabao jambo ambalo wamelifanyia kazi.

Kesho Agosti 20, Yanga itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya ASAS Djibouti katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex ambapo hata ule wa pili utachezwa pia Jumapili ijayo.

Kocha huyo amesema, “Mpira ni mchezo unahitaji mabao hivyo mchezo wetu wa kesho kutakuwa na mabadiliko.

“Tunatambua kwamba ushindani ni mkubwa na wapinzani wetu tunawaheshimu hivyo tuna amini kuwa tutafanya vizuri kupata matokeo.

“Kutakuwa na mabadiliko makubwa kwenye mchezo wetu nina amini mtakaojitokeza mtakuwa mashahidi,”.

Previous articleCHAMA NA LUIS NA JAMBO LINGINE
Next articleYANGA KUMEKUCHA, KIKOSI KUFUMULIWA