Home Sports CHAMA NA LUIS NA JAMBO LINGINE

CHAMA NA LUIS NA JAMBO LINGINE

MASTAA wa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu Robert Oliveira, Clatous Chama na Luis Miquissone wamekuja na jambo lingine katika kufunga na kutoa pasi za mabao.

Simba msimu wa 2022/23 walipishana na ubingwa ambao ulikwenda kwa watani zao wa jadi Yanga.

Pia hata taji la Ngao ya Jamii lilibebwa na Yanga na lile la Azam Sports Federation.

Wameanza kwa kutwaa taji ya Ngao ya Jamii kwa kupata ushindi dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa fainali uliochezwa Tanga, Uwanja wa Mkwakwani.

Wawili hao ambao ni viungo wamefungua akaunti za kuhusika katika mabao msimu mpya wa 2023/24.

Chama alifunga bao dhidi ya Mtibwa Sugar dakika ya 80 akitumia pasi ya Luis ambaye alianzia benchi Uwanja wa Manungu,

Baada ya kazi ya kukomba pointi tatu ugenini mbele ya Mtibwa Sugar kukamilika, Luis alibainisha kuwa ni furaha kwale kutoa pasi ya bao.

Chama akamwambia Luis kuwa anastahili pongezi lakini anapaswa kumtengenezea pasi zaidi.

“Hongera lakini nategemea kupata zaidi ya pasi 10 kutoka kwako msimu huu,”.

Kesho Agosti 20 Simba inatararajiwa kutupa kete ya pili dhidi ya Dodoma Jiji, Uwanja wa Uhuru

Previous articleSUALA LA KITAYOSCE TUACHE KUPEPESA WAMEKOSEA
Next articleYANGA YAJA NA HESABU NYINGINE