Home International CR 7 KUTOKA UARABUNI KUCHEZA UEFA

CR 7 KUTOKA UARABUNI KUCHEZA UEFA

CHAMA cha Soka Saudi Arabia kipo kwenye mazungumzo na UEFA kuhusu uwezekano wa bingwa wa Ligi Kuu ya Saudi Arabia kushiriki michuano hiyo msimu wa 2024/25.

Hii inakuja baada ya Saudi Arabia Pro League kusajili wachezaji wakubwa na waliokuwa vipenzi vya mashabiki wengi huko Ulaya.

Kwa sasa ligi ya Saudia imekuwa ikifuatiliwa tangu, Cristiano Ronaldo alipojiunga na Al Nassr ambayo inashiriki ligi hiyo na baada ya hapo ukafuata msururu wa nyota kibao majira haya ya joto kama, Karim Benzema (Al-Ittihad), Neymar (Al Hilal), Firmino (Al Ahli), Sadio
Mane (Al Nassr) na wengine kibao.

Uwepo wa mastaa hawa umewafanya mabosi wa Saudia kuangalia uwezekano wa klabu moja ambayo itaibuka bingwa kwenye ligi hiyo apate nafasi ya kushiriki Uefa 2024/25 jambo ambalo liko kwenye mchakato.

Iwapo pendekezo hili litakubaliwa na UEFA, huenda likawashuhudia wachezaji kama Cristiano Ronaldo, Karim Benzema na Neymar wakicheza Ulaya kwa mara nyingine.

Previous articleYANGA KUMEKUCHA, KIKOSI KUFUMULIWA
Next articleSIMBA MASTAA WAKE WASUKWA UPYA