Home Sports SIMBA MASTAA WAKE WASUKWA UPYA

SIMBA MASTAA WAKE WASUKWA UPYA

MASTAA wa Simba ikiwa ni pamoja na Luis Miquissone, Fabrince Ngoma, Jean Baleke na John Bocco wameanza kusukwa upya ili kurejea kwenye makali yao.

Nyota hao wameandika rekodi mbovu ya kukomba dakika 180 katika mechi za Ngao ya Jamii 2023 bila kufuga bao lolote licha ya kutwaa taji hilo.

Simba ilitwaa Ngao ya Jamii kwa ushindi wa penalti 3-1 dhidi ya Yanga baada ya dakika 90 kutoshana nguvu. Ikumbukwe kwamba katika mchezo wa hatua ya nusu fainali ya kwanza walishuhudia ubao wa Uwanja wa Mkwakwani ukisoma Simba 0-0 Singida Fountain Gate.

Sio washambuliaji pekee hata kinara wa kutengeneza pasi za mabao 2022/23 Chama aliyetoa pasi 14 kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Yanga alikwama kutoa pasi ya bao.

Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira amesema kuwa makosa ambayo yametokea katika Ngao ya Jamii watafanyia kazi kupata matokeo.

“Wachezaji wanajitahidi kutimiza majukumu yao na kutengeneza nafasi ambacho kimekosekana ni umaliziaji na hilo tunalifanyia kazi sehemu ya mazoezi tunaamini tutapata matokeo mazuri,”.

Mchezo wa kwanza kwenye ligi ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Manungu ukisoma Mtibwa Sugar 2-4 Simba na kituo kinachofuata ni Simba v Dodoma Jiji.

Previous articleCR 7 KUTOKA UARABUNI KUCHEZA UEFA
Next articleYANGA YAWEKA MTEGO CAF, KOCHA AMUONYA BALEKE SIMBA