Home Sports SIMBA YATWAA NGAO YA JAMII, SALIM SHUJAA

SIMBA YATWAA NGAO YA JAMII, SALIM SHUJAA

NGAO ya Jamii ni mali ya Simba baada ya kupata ushindi kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi ndani ya Uwanja wa Mkwakwani.

Ilikuwa ni fainali ambayo Yanga walikuwa na nafasi kubwa kwenye upande wa kupata matokeo ndani ya dakika 90 kutokana na mashambulizi waliyokuwa wakiyapeleka kwa Ally Salim.

Hilo pia limedhihirishwa na nahodha wa Yanga Bakari Mwamnyeto ambaye ameweka wazi kuwa hawakutumia nafasi walizopata.

Dakika 90 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga ubao umesoma Yanga 0-0 Simba na kupelekea wasake mshindi kwa penalti.

Simba imeshinda penalti 3-1 Yanga huku mpigaji akiwa ni Aziz Ki.

Kwa Simba Ally Salim ameibuka shujaa baadà ya kuzuia penalti tatu kuzama langoni mwake kutoka kwa Yanga.

Yanga chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamond inarejea Dar kuanza maandalizi ya msimu wa 2023/24 kwenye mechi za ligi na kimataifa.

Ikumbukwe kwamba Yanga walitwaa taji la Ngao ya Jamii 2022 kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba, Uwanja wa Mkapa.

Previous articleNGOMA NZITO MKWAKWANI TANGA: YANGA 0-0 SIMBA
Next articleSIMBA WAMESHINDA DHIDI YA TIMU ILIYOONYESHA UBORA