Home Sports NGOMA NZITO MKWAKWANI TANGA: YANGA 0-0 SIMBA

NGOMA NZITO MKWAKWANI TANGA: YANGA 0-0 SIMBA

DAKIKA 45 ubao wa Uwanja wa Mkwakwani mchezo wa Kariakoo Dabi unasoma Yanga 0-0 Simba.

Huu ni mchezo wa Ngao ya Jamii ikiwa ni fainali baada ya timu hizo kupenya hatua ya nusu fainali.

Clement Mzize na Kennedy Musonda hawa wameanza kwa ushambuliaji upande wa Yanga huku nahodha John Bocco akiongoza jahazi la Simba.

Eneo la kiungo vita ni kubwa kwa timu zote zikipambania kusepa na taji hilo la kwanza msimu wa 2023/24.

Djigui Diarra ni kwa upande wa Yanga yupo langoni na Ally Salim ni kwa upande wa Simba.

Previous articleKIKOSI CHA YANGA DHIDI YA SIMBA
Next articleSIMBA YATWAA NGAO YA JAMII, SALIM SHUJAA