Home Uncategorized MVUNJA PROTECTA BADO YUPO SANA AZAM

MVUNJA PROTECTA BADO YUPO SANA AZAM

MWAMBA Daniel Amoah beki wakuaminika ndani ya kikosi cha Azam FC bado yupo ndani ya Azam FC baada ya kuongeza dili la mwaka mmoja.

Nyota huyo anaingia kwenye orodha ya waliomtungua Djigui Diarra, ‘Screen Protecta’ kipa namba moja wa Yanga kwenye Mzizima Dabi, Uwanja wa Mkapa ubao uliposoma Azam FC 2-2 Yanga.

Amoah ni mechi 24 kacheza akiwa katupia mabao mawili ambapo bao la kwanza aliwatungua Yanga lingine aliwatungua Mtibwa Sugar, Uwanja wa Manungu.

Mbali na Amoah ambaye atakuwa ndani ya kikosi hicho mpaka 2025 beki mwingine ambaye yupo ndani ya kikosi hicho ni Malicko Ndoye.

Ndoye raia wa Senegal naye pia ameongeza dili la mwaka mmoja litakalomfanya adumu mpaka 2025 katika viunga vya Azam Complex.

Tayari Azam FC imetambulisha nyota wawili wapya ikiwa ni Feisal Salum kutoka Yanga pamoja na Gibril Silah raia wa Gambia.

Previous articleKIUNGO WA KAZI AMETUA AZAM FC
Next articleKIGOGO YANGA AFICHUA SIRI, WINGA MGHANA KATIKA RADA ZA SIMBA