Home Sports KIUNGO WA KAZI AMETUA AZAM FC

KIUNGO WA KAZI AMETUA AZAM FC

RASMI kiungo Djibril Sillah nyota wa Gambia ni ingizo jipya ndani ya Azam FC.

Kiungo huyo anakuja kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho ambacho kimekosa ubingwa msimu wa 2022/23 ambao umekwenda Yanga.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Azam FC imeweka wazi kuwa wamefikia makubaliano na Klabu ya RS Berkane kumnunua kiungo huyo mshambuliaji

Raia huyo wa Gambia anatarajiwa kutua hapahapa Kwa Nyerere muda wowote kuanzia sasa.

Msimu uliopita kwenye Ligi Kuu ya Morocco, Sillah alifanikiwa kufunga jumla ya mabao saba na kutoa pasi za mwisho nne, wakati akiwa kwa mkopo JS Soualem.

Previous articleVIDEO:JEMBE AFICHUA MKUDE KUSAJILIWA YANGA
Next articleMVUNJA PROTECTA BADO YUPO SANA AZAM