Home International LUKAKU AGOMEA OFA

LUKAKU AGOMEA OFA

STRAIKA Romelu Lukaku amegomea kujiunga na klabu za Saudi Arabia ambazo zimekuwa zikimwaga fedha nyingi kwa ajil ya kuzinasa saini za mastaa mbalimbali wa Ulaya.

Lukaku ameongeza kuwa anataka kuendelea kubakia Ulaya kwa kuichezea timu ya Inter Milan ambayo yupo kwa mkopo akitokea Chelsea ambayo ilimsajili kutokea klabuni hapo.

Klabu za Saudi Arabia zilikuwa zinamtaka nyota huyo kwa ajili ya kwenda kuungana na mastaa wenzake N’Golo Kante, Hakim Ziyech na Ruben Neves ambao wamesajiliwa na timu za nchi hizo ambapo walimtumia ofa mbili ambazo zote straika huyo alizikataa.

Rais wa Inter, Steven Zhang amethibitisha kuwa Lukaku, 30, anaipenda timu hiyo na watafanya mazungumzo na Chelsea kwa ajili ya mustakabali wa nyota huyo kikosini hapo.

Previous articleMUDA UMEWATENGANISHA SIMBA NA MKUDE
Next articleISHU YA MORRISON KUIBUKIA AZAM IPO HIVI