Home Sports YANGA YATWAA TAJI LA FA MKWAKWANI

YANGA YATWAA TAJI LA FA MKWAKWANI

NAHODHA wa Yanga Bakari Mwamnyeto ameshuhudia ubao wa Uwanja wa Mkwakwani ukisoma Azam FC 0-1 Yanga.

Bao pekee la ushindi kwa Yanga limepachikwa na Kennedy Musonda dakika ya 14 kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Mwamnyeto nahodha wa Yanga ametoka kushuhudia timu hiyo ikitwaa taji la Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2022/23.

Ni yeye kwa mara nyingine ameshuhudia timu hiyo ikisepa na taji la Azam Sports Federation kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Juni 12.

Anakuwa ni nahodha mzawa kuwa kwenye kikosi kilichotwaa mataji makubwa mawili na fainali dhidi ya timu bora Azam FC.

Ni Ngao ya Jamii, Ligi Kuu Bara na Azam Sports Federation wametwaa Yanga.

Musonda amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo leo Mkwakwani.

Previous articleNTIBANZOKIZA ATWAA TUZO YAKE
Next articleYANGA NA UBINGWA WA FA