Home Sports YANGA NA UBINGWA WA FA

YANGA NA UBINGWA WA FA

CEDRICK Kaze, kocha msaidizi wa Yanga amesema kuwa wachezaji wamejituma kucheza dhidi ya timu ngumu katika fainali.

Yanga imeshinda dhidi ya Azam FC kwenye fainali ya Kombe la Azam Sports Federation.

Ubao wa Uwanja wa Mkwakwani umesoma Azam FC 0-1 Yanga.

Mtupiaji ni Kennedy Musonda dakika ya 14 akifunga bao pekee ambalo limedumu mpaka mwisho wa mchezo.

Kaze amesema:” Ni timu kubwa na nzuri ambayo ni Azam tumecheza nayo hivyo pongezi kwa wachezaji kwa kazi kubwa.

“Furaha kubwa kuona tumepata ushindi na kutwaa taji hili kubwa,”.

Previous articleYANGA YATWAA TAJI LA FA MKWAKWANI
Next articleIJUE REKODI ALIYOFUNGA NAYO JOHN BOCCO