Home Sports IJUE REKODI ALIYOFUNGA NAYO JOHN BOCCO

IJUE REKODI ALIYOFUNGA NAYO JOHN BOCCO

NAHODHA wa Simba John Bocco amefunga msimu wa 2022/23 na rekodi yake a kufuta gundu ya kukwama kupachika bao ndani ya 2023.

Ipo wazi kuwa ni Desemba 30 2022 Bocco alifunga mabao kwenye mchezo wa kufungia mwaka kwa Simba alipowatungua mabao matatu Tanzania Prisons, Uwanja wa Mkapa.

Bocco alianza kwa kasi kwenye kucheka na nyavu alipokuwa akikimbizana na mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele ambaye kafunga msimu na mabao 17.

Baada ya kuukaribisha 2023 Bocco kwenye mechi ambazo alipata nafasi ya kucheza ikiwa ni pamoja na mchezo dhidi ya Azam FC, watani zao wa jadi Yanga alikwama kufunga.

Pia kwenye mchezo wa raundi ya 29 dhidi ya Polisi Tanzania alipoingia dakika ya 14 akichukua nafasi ya Jean Baleke alikwama kufunga kwenye mchezo huo.

Wakati wakifunga msimu kwa mchezo dhidi ya Coastal Union, Uwanja wa Uhuru, Bocco alibuka na kupachika bao moja wakati ubao uliposoma Simba 3-1 Coastal Union.

Hiyo ni baada ya kuyeyusha jumla ya siku 161 ndani yam waka 2023 kukwama kufunga ndipo akafunga bao lake ambalo linakuwa la 10 msimu huu.

Previous articleYANGA NA UBINGWA WA FA
Next articleKIKOSI BORA SIMBA WATAWALA, SINGIDA YAPENYA