Home Sports AZAM FC 0-1 YANGA

AZAM FC 0-1 YANGA

KENNEDY Musonda nyota wa Yanga amepachika bao la kuongoza kwa Yanga kwenye mchezo wa fainali ya Azam Sports Federation dhidi ya Azam FC.

Dakika ya 14 bao hilo limepachikwa na raia huyo wa Zambia ambaye aliwazidi ujanja mabeki wa Azam FC na kuandika bao kwa Yanga.

Uwanja wa Mkwakwani mashabiki wengi wamejitokeza kushuhudia mchezo wa leo ambao mmoja atasepa na taji hilo.

Ikumbukwe kwamba mabingwa watetezi wa taji hili ni Yanga.

Moja ya mchezo mzuri kwa kila timu kusaka ushindi ndani ya uwanja huku mbinu za kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza zikitumika.

Previous articleNGOMA ITAKUWA NZITO LEO UWANJA WA MKWAKWANI
Next articleNTIBANZOKIZA ATWAA TUZO YAKE