Home Uncategorized NGOMA ITAKUWA NZITO LEO UWANJA WA MKWAKWANI

NGOMA ITAKUWA NZITO LEO UWANJA WA MKWAKWANI

 CHAPCHAP ni sawa kwenye kufunga msimu wa 2022/23 lakini kazi itakuwa kubwa kwa wababe wawili, Uwanja wa Mkwakwani kusaka taji la Kombe la Azam Sports Federation.

Yanga wakiwa wametoka kwenye kilele cha furaha baada ya kutwaa taji la ligi wanakutana na Azam FC ambao hawajavuna taji msimu huu.

Hapa tunakuletea mtifuano utakavyokuwa:-

Wakali wakitokea benchi

Fiston Mayele anaingia kwenye orodha ya wakali wakitokea benchi alifanya hivyo kwenye mchezo dhidi ya Geita Gold, Singida Big Stars ambao ulikuwa ni wahatua ya nusu fainali.

Ilikuwa ni Mei 21,2023 dakika ya 82 alifunga bao pakee la ushindi lililoipeleka Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi kwenye fainali ambayo inatarajiwa kupigwa leo.

Hata mbele ya Geita Gold kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali alitokea benchi na kufunga bao la ushindi kwa Yanga.

Prince Dube anaingia kwenye orodha ya nyota wakali wakitokea benchi bao la ushindi dakika ya 73 aliwatungua Simba, Uwanja wa Nangwanda Sijaona alipochukua nafasi ya Idris Mbombo ambaye alipata maumivu kwenye mchezo huo.

Watakosekana

Jesus Moloko wa Yanga ataukosa mchezo huu kutokana na adhabu ya kadi nyekundu ambayo aliipata kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City ambao ulikuwa ni wa mzunguko wa 29, Uwanja wa Sokoine Mbeya.

Aziz KI na Mayele nao wanatajwa kuwa kwenye majukumu ya timu zao za taifa.

Vita ya taji

Yanga ni mabingwa watetezi wa taji hili la FA huku wakiwa na mataji kibao kwenye kabati lao wakitoka kuchukua Ligi Kuu Bara mara ya pili mfululizo baada ya kulitwaa msimu wa 2021/22 na msimu huu wa 2022/23.

Azam FC kabati lao ni hamna kitu msimu huu hivyo wakikosa na taji hili watakuwa wameambulia patupu kwa mara nyingine tena ndani ya 2022/23.

Mbinu matata

Ni mbinu za kocha msaidizi Kali Ongala ambaye ni mzawa dhidi ya Nasreddine Nabi ambaye ni raia wa Tunisia.

Dakika 90 zitaamua mbinu za kocha yupi zitatoa majibu kwa timu itakayotwaa ushindi wa kufungia msimu wa 2022/23.

Kila kocha ameweka wazi kuwa wanahitaji ushindi ili kutwaa taji hilo muhimu ndani ya Bongo.

Sopu na Diarra

Nyota pekee mwenye rekodi ya kumtungua mdaka mishale wa Yanga Djigui Diarra mabao mengi ndani ya msimu wa 2022/23 ni Abdul Suleiman, ‘Sopu’ ambaye alimtungua mabao mawili kwenye mchezo wa ligi.

Zama zile alipokuwa ndani ya Coastal Union kwenye mchezo wa fainali ya FA alimtungua Diarra mabao matatu akiwa ni nyota wa kwanza kufunga hat trick kwenye fainali. Je rekodi hiyo itajirudia sasa akiwa ndani ya Azam FC, basi subiri kwanza, jasho litamwagika.

Tuzo zinawahusu

Nyota wa Azam FC Prince Dube ambaye aliwatungua Simba kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali bao la ushindi Mei 7,2023 ubao wa Uwanja wa Nangwanda uliposoma Azam FC 2-1 Simba yupo kwenye orodha ya wanaowania tuzo.

Katika orodha iliyotolewa na Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF) wachezaji watano wameteuliwa kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports, (ASFC).

 Dube na Abdul Suleiman, ‘Sopu’ wote wa Azam FC, Bakari Mwamnyeto, Fiston Mayele na Clement Mzize wote wa Yanga hivyo mbali na vita ya kusaka taji pia kuna vita ya kusaka tuzo binfsi.

Ikumbukwe kwamba Sopu yupo pia kwenye orodha ya wanaowania tuzo ya mfungaji bora akiwa ametupia matatu na Mzize yeye ametupia mabao 6 kinara wa utupiaji ni Andrew Simchimba mali ya Ihefu akiwa ametupia mabao 7 lakini timu yake imegotea njiani.

Previous articleSIMBA WAIFUNIKA YANGA, AZAM FC
Next articleAZAM FC 0-1 YANGA