Home Sports SIMBA WAIFUNIKA YANGA, AZAM FC

SIMBA WAIFUNIKA YANGA, AZAM FC

MASTAA wa Simba wamewafunika watani zao wa jadi Yanga kwenye idadi ya hat trick ambazo wamefunga ndani ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Azam FC.

Msimu wa 2022/23 ni mastaa saba walifunga hat trick huku ikiwa ni watatu kutoka Simba, wawili kutoka Yanga  mmoja ni mali ya Namungo inayotumia Uwanja wa Majaliwa na aliyefunga kazi ni Prince Dube wa Azam FC.

Nyota wa kwanza kufunga hat trick msimu wa 2022/23 ni Fiston Mayele wa Yanga aliyefunga kwenye mchezo dhidi ya Singida Big Stars uliochezwa Uwanja wa Mkapa na alitoa pasi moja ya bao ikiwa ni pasi yake ya kwanza kati ya tatu.

Mwingine kufunga kutoka Yanga ni Aziz KI alifunga mchezo dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Uwanja wa Azam Complex huku akifunga mabao mawili kwa mapigo ya penalti.

Kutoka Simba ni John Bocco mwenye hat tick mbili aliwatungua Ruvu Shooting na Tanzania  Prisons mechi zte zilichezwa Uwanja wa Mkapa.

Jean Baleke wa Simba aliwatungua Mtibwa Sugar mchezo uliochezwa Uwanja wa Manungu, Morogoro.

Mwingine ni Saido Ntibanzokiza yeye anazo mbili aliwatungua Tanzania Prisons ikiwa ni mchezo wake wa kwanza ndani ya Simba akitokea Geita Gold na ile ya pili aliwatungua Polisi Tanzania, Uwanja wa Azam Complex.

Ibrahim Mkoko nyota wa Namungo aliwatungua KMC kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru waliposepa na pointi zote tatu mazima.

Prince Dube alifunga kazi kwa kufunga hat trick kwenye mchezo wa mwisho Juni 9 Uwanja wa Azam Complex alipowatungua Polisi Tanzania mabao manne na kufikisha mabao 12.

Jumla ndani ya Simba jumla hat trick zimefungwa tano huku Yanga ikiwa imefunga mbili na Namungo wanayo moja kabatini kama ilivyo Azam FC.

Previous articleNTIBANZOKIZA NA TUZO MKONONI, MABAO SABABU
Next articleNGOMA ITAKUWA NZITO LEO UWANJA WA MKWAKWANI