WINGA HUYU AINGIA ANGA ZA SIMBA

IMEELEZWA kuwa winga Leandre Onana mwenye miaka 23 mali ya Rayon Sports ya Rwanda yupo kwenye hesabu za mabosi wa Simba.

Timu hiyo imekosa taji la Ligi Kuu Bara ambao upo mikononi mwa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Nyota huyo ni winga ametupia mabao 15 na pasi 10 za mabao ametoa ndani ya timu hiyo.

Yote hayo ni katika Ligi Kuu ya Rwanda anatajwa kuwa kwenye rada za timu za Simba inayopambana kuboresha kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu Roberto Oliveira.

Oliveira hivi karibuni aliweka wazi kuwa alikwama kufanya vizuri kwenye mechi zake kutokana na uchovu wa wachezaji pamoja na majeraha kwa wachezaji.

“Tulikwama kupata matokeo kutokana na wachezaji kuwa wanasumbuliwa na majeraha na wengine walikuwa wanarejea taratibu kwenye ubora hivyo tukipata wachezaji wawiliwawili kwenye kila idara itakuwa bora,”.