Home Uncategorized HII NDIYO TIMU ATAKAYOCHEZA FEI TOTO

HII NDIYO TIMU ATAKAYOCHEZA FEI TOTO

INAELEZWA kuwa uongozi wa Yanga umeanza mazungumzo na Klabu ya Sekhukhume ya Afrika Kusini ili kufikia makubaliano ya kumuuza Feisal Salim.

Kiungo huyo mali ya Yanga yupo kwenye mvutano na mabosi wa timu hiyo ambayo Mei 28 itacheza fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger ya Algeria.

Taarifa zumeeleza kuwa busara za viongozi wa Yanga katikà kuokoa kipaji cha Feisal zimeamua iwe hivyo kijana acheze Kwa kuwa hataki kurejea Yanga na mkataba wake unagota mwisho 2024.

Desemba 24 2022 Fei aliwaaga mashabiki na viongozi kwa kusema Kwaherini Wananchi. Jambo hilo lilileta mvutano na mabosi wake wa Yanga ambao wameweka wazi kuwa nyota huyo hakufuata utaratibu kwenye kuvunja mkataba wake.

Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe aliweka wazi kuwa Feisal bado ni mchezaji wa Yanga na medali ambazo watachukua zote watamuwekea.

Previous articleWINGA HUYU AINGIA ANGA ZA SIMBA
Next articleBRIGHTON WANA BALAA UJUE WATOSHAN NGUVU NA TIMU BORA