Home Sports BOCCO NGOMA BADO NZITO

BOCCO NGOMA BADO NZITO

NAHODHA wa Simba, John Bocco ndani ya Ligi Kuu Bara ngoma bado ni nzito kwenye upande wa kucheka na nyavu.

Kinara wa utupiaji ni Fiston Mayele wa Yanga mwenye mabao 16 na pasi mbili za mabao.

Nahodha huyo mzawa ambaye ni mfungaji bora wa muda wote akiwa amefunga mabao zaidi ya 100 msimu huu kagotea kwenye mabao 9.

Bocco hajawa chaguo la kwanza chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira.

Simba imegotea nafasi ya pili kwenye ligi na vinara wakiwa ni Yanga ambao ni mabingwa msimu wa 2022/23.

Nyota huyo amesema kwenye mechi mbili ambazo zimebaki watapambana kuwapa furaha mashabiki.

Mchezo wao uliopita wakiwa Uwanja wa Azam Complex ubao ulisoma Simba 3-0 Ruvu Shooting ambayo itashiriki Championship msimu ujao.

Bocco amesema:”Tumeshindwa kufikia malengo yetu msimu huu tunafanya kazi kubwa kwa ajili ya kufanya vizuri msimu ujao na mechi ambazo zimebaki tutafanya kazi kubwa kupata matokeo,”,

Previous articleGALLANTS MARUMO 0-1 YANGA KIMATAIFA
Next articleAZAM FC YAIVUTIA KASI COASTAL UNION