Home Sports IHEFU WAIVUTIA KASI COASTAL UNION

IHEFU WAIVUTIA KASI COASTAL UNION

KLABU ya Ihefu imeanza hesabu kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union.

Ikumbukwe kwamba Ihefu inashikilia rekodi ya kuwa timu ya kwanza kuifunga Yanga kwa msimu wa 2022/23.

Yanga ni vinara wa ligi wakiwa na mechi tatu mkononi ambapo mchezo ujao ni dhidi ya Dodoma Jiji.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa jumapili, Uwanja wa Mkwakwani,Tanga.

Tayari kikosi hicho kimeanza maandalizi kuelekea mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Ofisa Habari wa Ihefu Peter Andrew amesema kuwa wachezaji wapo tayari na wanahitaji pointi tatu.

‘Maandalizi yameanza na wachezaji wana ari kubwa kuelekea mchezo wetu dhidi ya Coastal Union.

“Tunatambua kwamba utakuwa ni mchezo mgumu lakini tupo tayari na tunahitaji kupata pointi tatu,”.

Previous articleYANGA 0-0 GALLANTS MARUMO
Next articleYANGA MGUU MMOJA FAINALI KIMATAIFA