Home Uncategorized YANGA MGUU MMOJA FAINALI KIMATAIFA

YANGA MGUU MMOJA FAINALI KIMATAIFA

YANGA imetanguliza mguu mmoja hatua ya fainali kwa ushindi wa mabao 2-0 Marumo Gallants.

Kipindi cha pili Kocha Mkuu,Nasreddine Nabi amekamilisha kufunga hesabu kwa nyota wake kupachika mabao.

Ni Aziz KI kiungo wa Yanga alianza kutupia bao la ufunguzi dakika ya 63 kwa shuti akiwa ndani ya 18 na lile la pili ni mali ya mchetuaje Bernard Morison.

Morrison hakukata tamaa baada ya kuchezewa faulo na kipa pamoja na beki alikomaa na kupachika bao la pili dakika ya 90.

Mchezo wa nusu fainali ya pili utaamua mshindi atakayetinga hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Nabi alifanya mabadiliko kipindi cha pili ambayo yalikuwa na ngvu kwenye upande wa kiungo na kuongeza kasi ya ushambuliaji baada ya Mudhathir Yahya, Morrison kuingia,

Pia kwa upande wa ushambuliaji Clement Mzize aliongeza kitu na kuongeza makali eneo hilo akishirikiana na Fiston Mayele.

Previous articleIHEFU WAIVUTIA KASI COASTAL UNION
Next articleSISI WALEE, ONYANGO AOMBA KUONDOKA SIMBA