Home Sports YANGA 0-0 GALLANTS MARUMO

YANGA 0-0 GALLANTS MARUMO

HATUA ya nusu fainali ya kwanza Uwanja wa Mkapa, ubao unasoma Yanga 0-0 Marumo Gallants.

Dakika 45 za nguvu kwa Yanga ambao wanapambania kutinga hatua ya nusu fainali.

Kwenye upande wa viungo na ushambuliaji kazi kubwa inafanywa na Aziz KI, Tuisila Kisinda ambaye amekosa kwa kiasi fulani utulivu kutengeneza mashambulizi kwa Fiston Mayele.

Mayele anaonyesha kazi kwa Gallants akiwa ni nyota aliyepiga mashuti mengi kulenga lango la wapinzani wao ambayo ni manne.

Gallants imara kwenye kushambulia kwa kushtukiza huku wakiwa na kasi kulifuata lango la Yanga linalolindwa na Djigui Diarra ambaye anatimiza majukumu yake kwa umakini.

Mashabiki wamejitokeza kwa wingi Uwanja wa Mkapa kushuhudia burudani.

Previous articleMTIBWA SUGAR WAIVUTIA KASI POLISI TANZANIA
Next articleIHEFU WAIVUTIA KASI COASTAL UNION