Home International MANCHESTER UNITED WAPOTEZA POINTI JIONI

MANCHESTER UNITED WAPOTEZA POINTI JIONI

POINTI tatu za kikatili wamesepa nazo Brighton mbele ya Manchester united ambao walikuwa wanadhani wangeweza kupata angalau pointi moja ugenini.

Ubao wa Uwanja wa Falmer ulibadilika usomaji wake dakika ya 90+9 uliposoma Brigton 1-0 Man U.

Bao la pekee la ushindi mtupiaji ni Alexis Mac Allister aliwanyanyua mashabiki wa timu yake na kuwapa maumivu wale wa timu pinzani.

Kwenye mchezo huo ni mashuti 22 walipiga Brighton huku sita yakilenga lango na wapinzani wao walipiga mashuti 16 na matano yalilenga lango.

Pointi 55 kibindoni Brighton nafasi ya tano huku United ikiwa na pointi 63 nafasi ya nne.

Previous articleHUU HAPA MTAMBO WA MABAO MTIBWA SUGAR
Next articleVIDEO:ISHU YA SARE NAMUNGO SIMBA WACHARUKA