Home International SIMBA YAFUNGASHIWA VIRAGO LIGI YA MABINGWA AFRIKA

SIMBA YAFUNGASHIWA VIRAGO LIGI YA MABINGWA AFRIKA

NGOMA imegota mwisho kwa wawakilishi wa Tanzania Simba katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuondolewa na mabingwa watetezi wa taji hilo Wydad.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mohamed V umesoma Wydad Casablanca 1-0 Simba na kufanya matokeo ya jumla kuwa Wydad 1-1 Simba,

Ikumbukwe kwamba Simba ilipata ushindi wa bao 1-0 Uwanja wa Mkapa na imefungwa bao 1-0 Uwanja wa Mohamed V.

Katika mapigo ya penalti ni Wydad 4-3 Simba na kuwafanya wagotee wenye hatua hiyo mpaka wakati ujao wakipata nafasi kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

Previous articleWYDAD 1-0 SIMBA
Next articleHAYA NJOONI MJIFUNZE KWETU, SIMBA WAACHA GUMZO MOROCCO