Home Sports MAYELE ANA BALAA NA NYAVU HUYO

MAYELE ANA BALAA NA NYAVU HUYO

FISTON Mayele amefikisha jumla ya mabao 50 katika mashindano yote akiwa na kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Timu hiyo yenye maskani yake pale Jangwani inadhamiwa na kampuni ya SportPesa ambayo imeleta mapinduzi makubwa kwenye suala la michezo Bongo kwa kufungua njia kwa wadhamini wengine kuingia kuwekeza kwenye michezo.

Ikumbukwe kwamba Mayele amefunga mabao hayo ndani ya misimu miwili ambapo msimu wa kwanza ilikuwa ni 2021/22 na msimu wake wa pili ni 2022/23.

Msimu wake wa kwanza alipachika mabao 16 kwenye ligi rekodi huku msimu wa 2022/23 akifanikiwa kuandika rekodi ya mabao 16 kwenye ligi huku Yanga ikiwa na mechi nne mkononi.

Kete yake ya 50 alifikisha kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali alipofunga mabao mawili mchezo uliochezwa nchini Nigeria Apili 23, ubao uliposoma Rivers United 0-2 Yanga.

Mayele alipachika mabao hayo kipindi cha pili dakika ya 71 na 82 ambapo alitumia mguu wa kulia kuyajaza mabao hayo kimiani.

Pasi zote alitumia zilitoka kwenye miguu ya mzawa Bakari Mwamnyeto ambaye ni nahodha wa Yanga.

Mzee huyo wa kutetema ni chaguo la kwanza kwenye eneo la ushambuliaji anafikisha jumla ya mabao matano kwenye anga la kimataifa katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Previous articleShangwe Kubwa La Bodaboda Lasababishwa Na Meridianbet
Next articleCOASTAL UNION YASEPA NA POINTI TATU NA MBUZI MNYAMA