Home Sports COASTAL UNION YASEPA NA POINTI TATU NA MBUZI MNYAMA

COASTAL UNION YASEPA NA POINTI TATU NA MBUZI MNYAMA

TAWI la Coastal Union la ‘Obama Camp’ la Mabokweni Tanga, limetoa zawadi ya mbuzi mmoja kuwapongeza vijana wao kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Ushindi huo waliupata Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Bao la ushindi lilifungwa kiufundi na Gustava Simon kwa pigo la shuti kali akitumia mguu wa kushoto dakika ya 54.

Coastal Union wanafikisha pointi 30 nafasi ya 10 baada ya kucheza mechi 27, Mtibwa Sugar nafasi ya 11 pointi zao kibindoni ni 29.

Previous articleMAYELE ANA BALAA NA NYAVU HUYO
Next articleYANGA HAWAJARIDHIKA KABISA NA WALICHOPATA KIMATAIFA