Home Sports POLISI TANZANIA MAJANGA TUPU

POLISI TANZANIA MAJANGA TUPU

HAKUKUWA na usalama mkubwa kwa Polisi Tanzania walipokuwa ndani ya Uwanja wa Liti baada ya kuacha poiti zote tatu.

Ni majanga matupu kwa Polisi Tanzania wanaotafuta matumaini ya kucheza mchezo wa mtoano na kujinasua kutoka kwenye nafasi ya mwisho kwenye msimamo.

Aprili 7 ubao ulisoma Singida Big Stars ubao ulisoma Singida Big Stars 3–0 Polisi Tanzania.

Watupiaji walikuwa ni Pascal Wawa dakika ya 13,Nickosn Kibabage alipachika bonge moja ya bao dakika ya 57 huku msumari wa mwisho ukifungwa na Amiss Tambwe dakika ya 90.

Singida Big Stars inabaki nafasi ya tatu ikiwa na pointi 51 Polisi Tanzania nafasi ya 16 pointi zao ni 19 wote wamecheza mechi 26.

Previous articleAZAM FC YASEPA NA POINTI ZA MTIBWA SUGAR
Next articleVIDEO:SIMBA KUPANGWA NA WAYDAD JEMBE AFICHUA