Home Sports SIMBA KUWAKABILI IHEFU KWA TAHADHARI

SIMBA KUWAKABILI IHEFU KWA TAHADHARI

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa utawakabili wapinzani wao Ihefu kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali kwa tahadhari kubwa ili kupata matokeo mazuri.

Simba inatarajiwa kutupa kete yake leo mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex mshindi wa mchezo atakutana na Azam FC hatua ya nusu fainali.

Azam FC iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wanatambua wapinzani wao wanahitaji matokeo hivyo lazima wawaheshimu.

“Tunawatambua wapinzani wetu wanahitaji matokeo na ni timu inayoleta ushindani hivyo tutaingia kwa tahadhari kutafuta matokeo hasa ukizingatia kwamba tunahitaji kufika fainali.

“Haitawezekana kutinga fainali kama hakutakuwa na matokeo mazuri kwenye mechi amazo tunacheza, tangu awali tuliweka wazi kila timu ambayo tunakutana nayo tunakwenda kupambana nayo kwa umakini na hilo wachezaji wanalifanya katika hilo tunawapongeza,” amesema Ally.

Miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa kwenye mazoezi ya mwisho kuikabili Ihefu ni pamoja na nahodha John Bocco, Jean Baleke, Joash Onyango.

Previous articleYANGA:HATUNA MASHAKA KIMATAIFA, TUPO TAYARI
Next articleWIKIENDI YENYE ODDS KUBWA NDIO HII UNAWEZA KUWA MSHINDI WA TSH MILIONI 85 ZA JAKIPOTI