Home Sports YANGA KUITEKA MAZEMBE

YANGA KUITEKA MAZEMBE

MENEJA Walter Harrison ameweka wazi kuwa watawateka wapinzani wao TP Mazembe na kuchukua pointi tatu ugenini kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya makundi.

Leo Yanga ikiwa inaongoza kundi D na pointi 10 baada ya kucheza mechi tano ina kete ya mwisho dhidi ya TP Mazembe mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mazembe.

Ipo wazi kwamba kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Yanga 3-1 TP Mazembe hivyo mchezo wa leo Mazembe watakuwa wanahitaji kulipa kisasi na Yanga kulinda rekodi.

Walter Harrison, meneja wa Yanga amesema kuwa maandalizi yapo tayari na wanahitaji kupata pointi tatu kwenye mchezo huo ambao utakuwa mgumu.

“Tunahitaji kuiteka Mazembe na kuchukua pointi tatu ili kuweka rekodi ya kutinga hatua ya robo fainali tukiwa tunaongoza kundi pamoja na kufanya vizuri kwenye hatua inayofuata.

“Huu ni mchezo muhimu kwetu na wachezaji wanajua kwamba kila mmoja anahitaji ushindi, mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kwa wale ambao wapo hapa Lubumsbashi tunaomba wajitokeze kwa wingi kutushangilia,” .

Previous articleKIKOSI CHA YANGA DHIDI YA TP MAZEMBE
Next articleTP MAZEMBE 0-0 YANGA