Home Sports SIMBA MBELE YA RAJA CASABLANCA WAMETUNGULIWA NJE NDANI

SIMBA MBELE YA RAJA CASABLANCA WAMETUNGULIWA NJE NDANI

KWENYE hatua ya makundi dhidi ya Raja Casablanca Klabu ya Simba imepigwa nje ndani ndani ya dakika 180.

Mchezo ule uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Simba 0-3 Raja Casablanca na kuwafanya wapoteza pointi tatu mazima.

Kwenye mchezo wa pili uliochezwa ugenini ubao ulisoma Raja Casablanca 3-1 Simba.

Bao pekee la Simba limefungwa na Jean Baleke ambaye anafikisha mabao matatu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Manula katunguliwa mabao sita na Raja huku mabao mawili ikiwa ni kwa mikwaju ya penalti.

Simba ina kazi kubwa hatua ya robo fainali ambapo kwenye upande wa mabeki na ushambuliaji imekuwa bado ni tatizo huku kiungo angalau kwenye ushambuliaji ila kwenye ukabaji bado kidogo kunahitaji maoresho.

Previous articleCHAMPIONSHIP KUKIWASHA LEO
Next articleAZAM FC WAIVUTIA KASI MTIBWA SUGAR