Home Sports CHAMPIONSHIP KUKIWASHA LEO

CHAMPIONSHIP KUKIWASHA LEO

MWENYEKITI   wa Mbeya Kwanza, Mohamed Mashango  ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Championship dhidi ya Green Warrior Uwanja Majimaji,Ruvuma.

Mashango  amesema ” Tumejiandaa vizuri tunamshukuru Mungu kila kitu kinaendelea vizuri tumejipanga vizuri tunahitaji pointi tatu tunajua mchezo utakuwa mgumu tupo tayari kwa ajili ya kupambana .

“Hali ya wachezaji kwa ujumla ipo vizuri hakuna majeruhi wowote wachezaji wetu wana ari na morali kwa ajili ya mchezo wamejipanga vizuri kwa ajili ya kusaka alama tatu wanajua nini tunataka kwenye mchezo huu.

Mechi nyingine za mzunguko wa 25 leo itakuwa ni Pamba FC dhidi ya Kitayosce Uwanja wa Nyamagana.

Fountain Gate wao watacheza dhidi ya African Sports Uwanja wa CCM Gairo, JKT Tanzania dhidi ya Mbuni FC Uwanja wa Isamhuyo

Previous articleMASTAA YANGA WALA KIAPO, CAF YAWAPA JEURI SIMBA
Next articleSIMBA MBELE YA RAJA CASABLANCA WAMETUNGULIWA NJE NDANI