Home Sports AZAM FC WAIVUTIA KASI MTIBWA SUGAR

AZAM FC WAIVUTIA KASI MTIBWA SUGAR

BAADA ya kupoteza matumaini ya kutwaa taji la Ligi Kuu Bara,Azam FC imehamishia nguvu zake kwenye mashindano ya Azam Sports Federation.

Ni Aprili 3 itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo wa hatua ya robo fainali unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.

 Ofisa Habari wa Azam FC,Hasheem Ibwe alisema kuwa wanatambua umuhimu wa mashindano hayo na kila kitu kipo vizuri.

“Timu kubwa inafanya vitu vikubwa na kupata matokeo mazuri kwenye mechi zake hivyo nasi tunajipanga kufanya mambo makubwa kwa kupata matokeo mazuri.

“Safari hii tumedhamiria kufanya kweli kwenye Kombe la Azam Sports Federation ndio maana tulianza kupata ushindi mkubwa kwenye mechi zile za mwanzo ipo wazi ikumbukwe tuliwafunga Malimao mabao mengi, ” amesema Ibwe.

Previous articleSIMBA MBELE YA RAJA CASABLANCA WAMETUNGULIWA NJE NDANI
Next articleMAN CITY YAICHAPA 4G LIVERPOOL