Home International SIMBA KUIVAA RAJA CASABLANCA LEO

SIMBA KUIVAA RAJA CASABLANCA LEO

MCHEZO wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya Raja Casablanca ni leo Machi 31 nchini Morocco.

Mchezo huo unachezwa Morocco ikiwa ni Machi 31 lakini Tanzania itakuwa ni Aprili Mosi 2023.

Ni mchezo wa mwisho hatua ya makundi kwa timu hizi mbili ambazo zote zimetinga hatua ya robo fainali.

Simba inakumbuka mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Simba 0-3 Raja Casablanca.

Ahmed Ally Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa mechi hiyo ni ya rekodi kwa kuwa ni mwanzo na mwisho wa mwezi.

“Ni mchezo wa rekodi unachezwa mwisho wa mwezi Machi kwa Morocco na mwanzo wa mwezi ikiwa ni Aprili Mosi kwa Tanzania,”.

Wachezaji wa Simba Machi 30 walifanya mazoezi ya mwisho ikiwa ni pamoja na beki Joash Onyango, Jean Baleke, Moses Phiri,Kenned Juma.

Previous articleVIDEO:MWAKINYO HUYU HAPA MSIKIE KUHUSU PAMBANO LAKE
Next articleKIMATAIFA, MWENDO WA KUSAKA REKODI