Home Uncategorized YANGA YAWAITA MASHABIKI KWA MKAPA

YANGA YAWAITA MASHABIKI KWA MKAPA

ALI Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema ni muhimu kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Mkapa kushuhudia kazi dhidi ya US Monastir.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Jumapili ambapo kwa sasa tiketi zinaendelea kuuzwa.

Kwenye muda wa hamasa mashabiki wa Yanga wamepata fursa ya kuzungumza na wachezaji wa timu hiyo kwa njia ya simu.

Kamwe amesema:”Mashabiki wana nguvu kubwa na tunawahitaji Uwanja wa Mkapa kwa ajili ya mchezo wetu ambao una tiketi yetu ya kutinga robo fainali Kombe la Shirikisho Afrika.

“Tuna kila sababu ya kufanya vizuri hasa ukizingatia tutakuwa nyumbani kikubwa ni kila mmoja kujitokeza kwa wingi na kupata tiketi yake mapema.

“Mchezo utakuwa mgumu lakini benchi la ufundi lipo tayari kwa ajili ya kutoa burudani na ushindi ndani ya dakika 90,”.

Previous articleKAGERA SUGAR KUJIPANGA UPYA
Next articleTABASAMU KIMATAIFA LINAHITAJIKA