TABASAMU KIMATAIFA LINAHITAJIKA

  MBALI kimataifa kila mchezaji anapenda kuona timu yake inafika hata mashabiki pia wanafikiria jambo hilo hasa ukizingatia kwamba mechi zinazofuata zinachezwa Uwanja wa Mkapa.

  Kuna furaha kubwa kwenye mechi za kimataifa zinapochezwa Uwanja wa Mkapa mbele ya mashabiki wa timu husika ambao wamekuwa wakijotokeza kwa wingi.

  Hakika katika hili ni muhimu kila mmoja kuguswa na kufanya kwa vitendo ikiwa atakuwa na muda wa kwenda uwanjani afike bila kukosa.

  Itaongeza deni kwa wachezaji kucheza kwa juhudi na kusaka ushindi ndani ya dakika 90 kwenye mechi za kimataifa jambo ambalo linawezakana.

  Ukubwa wa mashindano haya uendane na matokeo ambayo yatapatikana na uzuri ni kwamba kila mchezaji anapenda kupata matokeo mazuri.

  Basi ikawe hivyo kwenye mechi ambazo zinatarajiwa kuchezwa wikeendi hii ya Machi itakayowafanya wale wawakilishi wa kimataifa kuwa kazini.

  Kuanzia mashabiki, benchi la ufundi kila mmoja atimize jukumu lake bilakuwasahau wachezaji ambao hawa ni watu wa mwisho kukamilisha mpango kazi.

  Kuna wachezaji ambao wamekuwa wakicheza chini ya kiwango mechi za kimataifa kwa mechi hizi zilizobaki wasikubali kucheza chini ya kiwango.

  Inatokea siku unakwama kucheza vizuri lakini ukiweka nia mapema kabla ya mchezo hata ukiwa kwenye siku mbaya kazini bado utafanikiwa kucheza kwa umakini.

  Hakika wakati uliopo ni sasa na inawezekana kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake na kazi ikawa ni nzuri mwisho tabasamu likahusika kwa kila mmoja.

  Uzuri ni kwamba tabasamu huwa linatokea mwisho hivyo mwanzo kuna maumivu makubwa ambayo ni muhimu kuyafanyia kazi.

  Previous articleYANGA YAWAITA MASHABIKI KWA MKAPA
  Next articleINFANTINO ACHAGULIWA TENA KUONGOZA FIFA