Home Uncategorized KAGERA SUGAR KUJIPANGA UPYA

KAGERA SUGAR KUJIPANGA UPYA

KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa watajipanga kwa mechi zijazo ili kupata matokeo mazuri.

Timu hiyo kwenye mchezo uliopita ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya KMC uliochezwa Uwanja wa Uhuru.

Maxime amesema kuwa kuna kazi kubwa ya kuwaandaa wachezaji wake kupata matokeo mazuri kwenye mechi za ligi na wanaamini watarejea kwenye ubora.

“Kila mchezaji anatimiza majukumu yake kwa umakini na hili linanifurahisha, kwenye mechi ambazo tunapoteza bado wachezaji wanacheza kwa umakini mkubwa na burudani inaonekana.

“Kwa mechi zijazo tutafanyia kazi makosa yetu ili kufanya vizuri mechi zetu kwani ligi ina ushindani mkubwa nasi tunahitaji pointi tatu muhimu katika mechi ambazo tunacheza mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,”.

Kwenye msimamo Kagera Sugar ipo nafasi ya 7 ia pointi 32 kibindoni.

Mchezo wao ujao unatarajiwa kuwa dhidi ya Yanga Aprili 7,2023 Uwanja wa Azam Complex.

Ule wa mzunguko wa kwanza, Kagera Sugar ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na mtupiaji alikuwa ni Bernard Morrison.

Previous articleROBERTINHO AWAFANYIA UMAFIA HOROYA,YANGA YAWAKOMALIA WAARABU
Next articleYANGA YAWAITA MASHABIKI KWA MKAPA