Home International SENEGAL NDANI YA BONGO

SENEGAL NDANI YA BONGO

INAINGIA kwenye rekodi mpya ndani ya Bongo kwa mchezaji anayecheza Ligi Kuu Bara kuitwa timu ya Taifa ya Senegal.

Ni Pape Ousmane Sakho ameitwa kwenye Timu ya Taifa ya Senegal kwenda kujumuika na wenzake kwaajili ya maandalizi ya mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu AFCON 2023 dhidi ya Msumbiji.

Sakho bado hajawa kwenye mwendo mzuri ndani ya kikosi cha Simba kutokana na uwezo wake kuwa ni maji kupwa maji kujaa licha ya uwezo mkubwa alionao.

Ana kazi kubwa ya kufanya atakapopewa nafasi kwenye Timu ya Taifa ya Senegal moja ya sehemu yenye soka la ushindani mkubwa ambapo anaungana na staa mpenda watu Sadio Mane.

Wachezaji wengine wa Simba walioitwa kwenye timu zao za taifa mpaka sasa ni Henock Inonga (DR Congo), Clatous Chama (Zambia), Aishi Manula, Mzamiru Yassin, Beno Kakolanya (Tanzania).

Previous articleSIMBA WAIPIGIA HESAU ROBO FAINALI
Next articleWIKENDI HII TUSUA PESA UKIWA NA MERIDIANBET, VIWANJA MBALIMBALI KITAWAKA