Home Sports SIMBA WAIPIGIA HESAU ROBO FAINALI

SIMBA WAIPIGIA HESAU ROBO FAINALI

BEKI mwenye uwezo wa kupandisha na kulinda lango la Simba, Shomari Kapombe ameweka wazi kuwa watapambana kufikia malengo ya kutinga hatua ya robo fainali.

Simba ikiwa imecheza mechi nne za hatua ya makundi, Kapombe ameanza zote kikosi cha kwanza huku akishuhudia timu hiyo ikifungwa mabao manne na wao wakifunga mabao mawili.

Mchezo wao dhidi ya Horoya Uwanja wa Mkapa Machi 18.Mchezo wa kwanza uliochezwa Guinea Simba ilipoteza kwa kutunguliwa bao moja, nafasi ya pili ikiwa na pointi 6 vinara ni Raja Casablanca wenye pointi 12.

Kapombe amesema kuwa kazi ni kubwa kwenye mechi za kimataifa na wanapambana kupata matokeo.

“Sio kazi rahisi kwenye mashaindano ya kimataifa kupata matokeo mazuri ambacho tunakifanya ni maandalizi na kufuata maelekezo ya benchi la ufundi.

“Nina amini kwa mechi ambazo tunacheza tunazidi kuwa imara hivyo tutapambana kupata matokeo mazuri mashabiji wazidikuwa pamoja nasi,” .

Horoya wao wapo nafasi ya tatu wakiwa na pointi nne na wale Vipers wapo nafasi ya nne wakiwa wamesepa na pointi moja kibindoni.

Kesho Uwanja wa Mkapa kazi hiyo inatarajiwa kufanyika amapo timu zote zinasaka pointi tatu muhimu.

Previous articleRUVU SHOOTING:TUNACHUKUA POINTI KWENYE UGUMU
Next articleSENEGAL NDANI YA BONGO