Home Sports RUVU SHOOTING:TUNACHUKUA POINTI KWENYE UGUMU

RUVU SHOOTING:TUNACHUKUA POINTI KWENYE UGUMU

MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting amesema kuwa mwendo wa mpapaso utaendelea kwenye mechi zilizobaki licha ya kuwa zitakuwa ngumu hawana mashaka.

Timu hiyo haijawa kwenye mwendo mzuri Februari 17 ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Nyankumbu ukisoma Geita Gold 3-2 Ruvu Shooting na Februari 24 ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Jamhuri, Moro ukisoma Ruvu Shooting 0-1 Kagera Sugar.

 Machi 10 ubao wa Uwanja wa Sokoine ulisoma Mbeya City 1-2 Ruvu Shooting na pointi tatu walisepa nazo ugenini wakifikisha pointi 20 nafasi ya 15 baada ya kucheza mechi 25.

 Bwire amesema:”Tuna kazi kubwa ya kufanya ukizingatia ushindani ni mkubwa nasi tunataka kuchukua pointi tatu kwenye ugumu ambao tunakutana nao.

“Tuna wachezaji wazuri na wenye ari ya kusaka ushindi tuna amini kwa mechi ambazo zimesalia kazi itakuwa kubwa kwenye kusaka ushindi na inawezekana,”.

Ikumbwe kwamba mchezo wao dhidi ya KMC uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro walisepa na pointi tatu mazima.

Previous articleVIDEO;SIMBA YAWEKA WAZI MIPANGO KUIKABILI HOROYA
Next articleSIMBA WAIPIGIA HESAU ROBO FAINALI