Home Uncategorized KUMBE GEITA GOLD WALIPANGIWA KOSI LA CAF MECHI YA LIGI

KUMBE GEITA GOLD WALIPANGIWA KOSI LA CAF MECHI YA LIGI

BAADA ya Geita Gold kuambulia kipigo cha mabao 3-1  kutoka kwa Yanga ,Mkurugenzi wa  Geita Gold Zahar  Michuzi  amefunguka na kusema kuwa Yanga  waliwapangia kikosi cha CAF.

Mchezo huo ulipigwa  wikiendi hii Jumapili  kwenye Uwanja wa Chamazi ambapo Geita Gold ilianza kufunga kisha ikakwama kushinda mchezo huo.

Mwenyeketi wa Geita Gold Zahar amesema “Kitendo cha Yanga kutuwekea kikosi cha  CAF kwa timu yetu ya Geita Gold  iliyotoka  Buseresere  ni shambulio la aibu  kwa sababu haiwezekani  kikosi cha CAF tuchezeshwe  sisi utafikiri wanacheza  Shirikisho?

“Kulikuwa na haja gani ya kufanya hayo yote hayo tunaweza tunawamudu isipokuwa  bahati ili kuwa siyo kwetu  mchezo ulikuwa mzuri  pande zote  lakini sisi tulikosa matokeo,” .

Geita Gold imepoteza mechi zote mbili dhidi ya Yanga ule wa awali ilifungwa bao 1-0 Uwanja wa CCM Kirumba na mzunguko wa pili walifungwa mabao 3-1.

ReplyForward

Previous articleSIMBA KAMILI KIMATAIFA, JEMBE LA KAZI LAJUMUISHWA KIKOSINI
Next articleCITY YAPIGA MTU KIFURUSHI CHA WIKI